Posts

Showing posts from July, 2014

WASICHANA 60 WAKWEPA BOKO HARAM

Image
wasichana waliotekwa na Boko Haram Maafisa wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara. Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao. wapiganaji wa Boko Haram Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa. Bado wasichana wengine hawajapatikana Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ...

SHAMBULIZI LAFANYIKA PWANI YA KENYA

Image
Mashambulizi katika eneo la Mpeketoni kenya Kuna Ripoti ya mashambulizi matatu katika maeneo ya pwani ya kenya karibu na mpaka wa kenya na Somali.  Maafisa wa polisi wilayani Lamu wanachunguza milio mikali ya risasi iliosikika katika kituo kimoja cha kibiashara karibu na mji wa Mpeketoni ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa katika mashambulizi mawili mwezi uliopita. Kusini mwa Mpeketoni, kituo kimoja cha polisi katika wilaya ya Tanaraiver kinadaiwa kushambuliwa huku baadhi ya nyumba zikichomwa. Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo bila ya kutoa maelezo zaidi. Mwandishi wa BBC nchini kenya amesema kuwa kuna polisi wengi katika maeneo ya pwani kufuatia shambulizi hilo la mwezi uliopita.

NEYMAR KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Image
Mchezaji Neymar baada ya kupata jeraha Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha. Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia. Taarifa zinazohusiana        Michezo Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika. Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu. Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano. Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao. Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

Mama amtelekeza mtoto ndani ya karatasi

Image
Mwanamke mmoja aliyemtelekeza mwanawe ndani ya karatasi ya plastiki katika bustani moja nchini Uingereza aponea adhabu ya kifungo jela. Mtoto huyo mchanga aliyekuwa wa siku moja tu, alipatwa na mtu aliyekuwa anamtembeza Mbwa wake katika bustani hilo. Taarifa zinazohusiana  UINGEREZA Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita na kuwekwa chini ya ulinzi wa maafisa wa kijamii kwa miaka miwili.   Hata hivyo alikiri kumtelekeza mtoto wake kwa maksudi na kusema kuwa aliathirika kimawazo baada ya kujifungua mtoto huyo mwezi Mei. Polisi walisema kuwa mtoto huyo alinusurika kifo kwa dakika thelathini tangu kutelekezwa kwani alipatikana haraka sana na kwamba mwili wake tayari ilikuwa umeanza kuwa baridi. Mtoto huyo alipat...

Brazil inahitaji mwanasaikolojia

Image
Wachezaji wa Brazil baada ya kushinda Chile kupitia tundu la sindano Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari ameagiza mwanasaikolojia kujiunga na kambi ya mazoezi ya timu hiyo kufuatia ushindi mgumu dhidi ya mahasimu wao wakuu Chile. Wenyeji hao wa kombe la dunia walihitaji muda wa zaida na bahati kuilaza Chile mabao 3-2 jambo lililowaacha wengi wa wachezaji wao akiwemo Neymar wakitoa machozi baada ya mechi hiyo katika uwanja wa Estadio Mineirao. Taarifa zinazohusiana 1.BRAZIL 2.MICHEZO Neymar alisema "mechi hiyo dhidi ya Chile ilikuwa na umuhimu mkubwa kwetu katika azimio letu la kuffuzu kwa fainali ya mashindano hayo kwa hivyo haikuwa udhaifu ni machozi ya furaha'' Brazil atachuana na Colombia katika robo fainali siku ya ijumaa. Matumaini ya wenyeji ni kuwa Neymar ataiongoza timu hiyo kunyakua kombe la dunia . Mshambulizi huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 22 tayari ameifungia timu yake mabao manne.

Wachezaji wa Ujerumani waugua mafua

Image
Wachezaji saba wa Ujerumani, wanaugua mafua , saa 24 kabla ya mechi yao ya robo fainali dhidi ya Ufaransa. Kocha Joachim Low anasema kuwa wengi wanaumwa na koo ingawa hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa. Taarifa zinazohusiana        MICHEZO "ni mapema sana kufanya uamuzi wowote kuhusu orodha ya wachezaji watakaoingia uwanjani, '' alisema Low Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria Jumatatu. Low anaamini kuwa mazingira ya Brazil na safari za hapa na pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu ya wachezaji wake kuugua. Lakini aliongeza kuwa , hali sio mbaya sana , sitaki watu wadhani kuwa tunakabiliwa na wakati mgumu, hapana, '' alinukuliwa akisema Low