NEYMAR KUKOSA KOMBE LA DUNIA
Mchezaji Neymar baada ya kupata
jeraha
Nyota wa timu ya soka ya Brazil
Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa
mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Taarifa
zinazohusiana
Michezo
Neymar aligongwa upande wake wa
nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa
katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki
katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu
fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar
kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea
ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza
Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .
Comments
Post a Comment