Wachezaji wa Ujerumani waugua mafua
Wachezaji saba wa Ujerumani,
wanaugua mafua , saa 24 kabla ya mechi yao ya robo fainali dhidi ya Ufaransa.
Kocha Joachim Low anasema kuwa wengi
wanaumwa na koo ingawa hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa.
Taarifa
zinazohusiana
MICHEZO
"ni mapema sana kufanya uamuzi
wowote kuhusu orodha ya wachezaji watakaoingia uwanjani, '' alisema Low
Mats Hummels na Christoph Kramer
waliugua mapema wiki hii huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria
Jumatatu.
Low anaamini kuwa mazingira ya
Brazil na safari za hapa na pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu
ya wachezaji wake kuugua.
Lakini aliongeza kuwa , hali sio
mbaya sana , sitaki watu wadhani kuwa tunakabiliwa na wakati mgumu, hapana, ''
alinukuliwa akisema Low
Comments
Post a Comment