Brazil inahitaji mwanasaikolojia
Wachezaji wa Brazil baada ya
kushinda Chile kupitia tundu la sindano
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari
ameagiza mwanasaikolojia kujiunga na kambi ya mazoezi ya timu hiyo kufuatia
ushindi mgumu dhidi ya mahasimu wao wakuu Chile.
Wenyeji hao wa kombe la dunia
walihitaji muda wa zaida na bahati kuilaza Chile mabao 3-2 jambo lililowaacha
wengi wa wachezaji wao akiwemo Neymar wakitoa machozi baada ya mechi hiyo
katika uwanja wa Estadio Mineirao.
Taarifa
zinazohusiana
1.BRAZIL
2.MICHEZO
Neymar alisema "mechi hiyo
dhidi ya Chile ilikuwa na umuhimu mkubwa kwetu katika azimio letu la kuffuzu
kwa fainali ya mashindano hayo kwa hivyo haikuwa udhaifu ni machozi ya furaha''
Brazil atachuana na Colombia katika
robo fainali siku ya ijumaa.
Matumaini ya wenyeji ni kuwa Neymar
ataiongoza timu hiyo kunyakua kombe la dunia .
Mshambulizi huyo wa Barcelona mwenye
umri wa miaka 22 tayari ameifungia timu yake mabao manne.
Comments
Post a Comment