WASICHANA 60 WAKWEPA BOKO HARAM
wasichana waliotekwa na Boko Haram
Maafisa wa usalama wa Nigeria
wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa
kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa
miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa
kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria imeitisha kufanywe
uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
wapiganaji wa Boko Haram
Baadhi ya vyombo vya habari nchini
humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji
nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria
amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50
karibu na mji wa Damboa.
Bado
wasichana wengine hawajapatikana
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa
Boko Haram wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi
Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya
mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia
serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.
Comments
Post a Comment