MWACHENI MAMA AITWE MAMA

Imekuwa kawaida kuwa kila ifikapo tarehe 8 ya mwezi wa tatu tunaazimisha siku ya mwanamke Duniani kwa sababu mama ndio kiungo muhimu katika familia maana yeye ndiye ana kazi kubwa ya malezi tangu mtoto yupo tumboni hadi anakuwa kwaiyo mama ananafasi kubwa katika familia. Mueshimu mama ili hupate misingi mizuri ya kujua kuishi na watu pamoja kuwa na akili iliyo thabiti maana bila mama baba asingepata jina la baba fulan. Kwaiyo tunapo azimisha sherehe hiyo ya siku ya mwanamke Duniani lazima tutambue kuwa bila ya mama bado atujakamilika . Yoteyote tuwaeshimu mama zetu ili tuweze kupata hekima ya maisha marefu duniani na siku zote za maisha mpe nafasi mama maana yeye ndio anajua uchungu wa mwana. Tuwapende mama zetu ili tupate miaka mingi na heri duniani.