Posts

Showing posts from February, 2014

Wote kwa pamoja tushabikie yanga

Image
Chamsingi kuungana mashabiki wa timu zote tuache usimba na uyanga maana aujengi maendeleo ya kimpira katika nchi yetu ya Tanzania twendeni uwanja Taifa kesho 1.03.2014 yanga hoyeeeeeeee

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY

Image
  Hatimaye muda umefika. Al Ahly tayari wapo jijini. Kwa mashabiki wa Yanga, ni wakati wa hisia mchanganyiko. Furaha iliyojichovya kwenye woga wa kukutana na timu kubwa. Kwa upande mmoja wasingependa kukutana na wababe wao katika raundi ya kwanza. Kwa upande wa pili, timu kubwa kama Alhly hupandisha mzuka kwa mashabiki. Ni fursa nyingine tena kwa Yanga, aidha kufungua ukurasa mpya kwa kuwafunga wamisri kwa mara ya kwanza au kuendeleza uteja kwa waarabu. Mechi sita, vipigo vinne, kapu la magoli 14 huku wakijitutumua kwa kufunga bao moja ni historia ambayo kila Mwanajangwani asingependa iendelee hio Jumamosi. Mara ya mwisho, timu hizi zilipokutana, Al Ahly walimaliza biashara kwenye mechi ya kwanza tu kwa ushindi wa 3-0 huko Cairo. Kipigo cha ‘tatu bila’ kilipelekea kocha wa Yanga wa wakati huo, Dusan Kondic kuinua mikono na kukiri ‘kiroho safi’ tu kuwa Al Ahly wapo anga zingine na Yanga hawawezi kushinda hata mechi ya marudiano nyumbani. Mechi ya marudiano hapa Dar,...

TFF YAJIPANGA KUKUZA WATOTO KWENYE MICHEZO

Image
Rais wa shirikisho la mpira   Nchini Tanzania TFF,JAMAL MALINZI amesema kuwa anampango wa kukuza vipaji kwa vijana wa Tanzania ili kuweza kupata timu ya Taifa iliyo kamilika ilikuweza kufika mafanikio na malengo ya kutaka kucheza kombe la dunia mwaka 2018 ameyasema hayo alipotembelea shule za kukuza vipaji jijini mwanza akiambatana na viongozi wenzie katika msafara huo. Amesema kuwa lengo ni kufika mbali kisoka katika nchi ya Tanzania “Nina mpango wa kuleta maendeleo katika ya kimpira katika nchi ya Tanzania sababu ni kuweka mikakati ili kuweza kufanikiwa katika viwango vya juu kisoka ili kuleta mabadiliko katika nchi yetu” Pamoja na kusema hayo rais wa TFF pia akasema kuwa ni lazima tupiganie kuweza kufika mafanikio ya kimpira katika nchi yetu na kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele akishirikiana na viongozi wenzake ili kuwezesha kupata timu za Taifa zote kwa upande wa wavulava na wasichana . Rais wa shirikisho ameendelea kusema kuwa”lakini lazima ku...

Okwi ni noma sana

Image
Okwi akifanya yake kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salaam wakati akicheza  Ruvu shooting na kufanikiwa kufunga bao moja katika mchezo huo.

Siku ya wapenda nao ya tarehe 14/02/2014

Ni siku ambayo ilikuwa inasubiliwa sana kwa wale ambao wapo katika mahusiano ya kimapenzi lakini ata wale ambao wanapenda marafiki zao pamoja na wazazi. Pamoja kufurahia mahusiano ya na familia zingine na katika jamii zingine   tunaoishi nao kila siku katika maisha yetu kitu cha msingi kuishi kwa amani na upendo na watu katika jamii zetu. Pamoja tunaweza tukaendelea kuishi kwa amani na upendo katika maisha yetu valentine njema.

Macho na masikio kwenu Azam na Yanga.

Vilabu viwili vya Tanzania bara Azam fc na Yanga ndivyo zilizopata jukumu la kushirik katika michuano ya Klabu bingwa Afrika.   Ushiriki wa vilabu hivyo umekuja baada ya vilabu hivyo kufanya vizuri katika michezo yao ya mwanzo ambazo Yanga ilishinda mabao 7-0 ilipokutana na wacomoro kutoka katika visiwa vya Comoro. Azam nayo ilishinda kwa bao 1-0 pale ilipochuana vikali na Klabu moja kutoka Msumbiji. Matokeo hayo yameziwezesha timu hazo kuiwakilisha Tanzania katika kushiriki michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ambapo Yanga itamenyana kwa mara ya pili na Wacomoro hao katika visiwa hivyo. Azam nao wanatarajiwa kushuka dimbani siku ya jumapili hiihuko Msumbiji dhidi ya wanamsumbiji kwa mechi ya marudiano wakitafuta kucheza 16 bora ili waweze kuendelea na michuano hiyo. Macho na masikio ya watanzania ni kwa timu hizo mbili kurudi na ushindi ili waweze kuingia katika michuano hiyo ya timu 16 bora.