TFF YAJIPANGA KUKUZA WATOTO KWENYE MICHEZO





Rais wa shirikisho la mpira  Nchini Tanzania TFF,JAMAL MALINZI amesema kuwa anampango wa kukuza vipaji kwa vijana wa Tanzania ili kuweza kupata timu ya Taifa iliyo kamilika ilikuweza kufika mafanikio na malengo ya kutaka kucheza kombe la dunia mwaka 2018 ameyasema hayo alipotembelea shule za kukuza vipaji jijini mwanza akiambatana na viongozi wenzie katika msafara huo.





Amesema kuwa lengo ni kufika mbali kisoka katika nchi ya Tanzania “Nina mpango wa kuleta maendeleo katika ya kimpira katika nchi ya Tanzania sababu ni kuweka mikakati ili kuweza kufanikiwa katika viwango vya juu kisoka ili kuleta mabadiliko katika nchi yetu”

Pamoja na kusema hayo rais wa TFF pia akasema kuwa ni lazima tupiganie kuweza kufika mafanikio ya kimpira katika nchi yetu na kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele akishirikiana na viongozi wenzake ili kuwezesha kupata timu za Taifa zote kwa upande wa wavulava na wasichana .

Rais wa shirikisho ameendelea kusema kuwa”lakini lazima kuwa na mikakati na mlengo muhimu ili kuweza kufika mbali kisoka kwa sababu ukiwa malengo ni lazima ufanye kwa ubunifu zaidi ili kupata vitu vizuri kwe mpira na ni wakati wa kubadilika kimawazo maana viongozi waliopita katika shirikisho hili la mpira walikuwa wa maneno na sio vitendo zaidi”.

Hatimaye  tutaweza kubadilika kwa sababu tumejipanga vizuri katika swala la kukuza vipaji katika nchi yetu ili nasi tujivunie mafanikio katika soka la Tanzania kwa kujitangaza kimataifa na tukifikia katika malengo hayo nasi tutakuwa tunaweza kushindana katika mashindano ya ndani ya nchi yetu na yale nje ya nchi.

Pamoja na hayo yote na serikali iko pamoja nasi kuakikisha kuwa tunafika malengo ya kufanikiwa  na kuweza kujimudu wenyewe ili kuendeleza swala la mpira katika nchi yetu ya Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY