Macho na masikio kwenu Azam na Yanga.
Vilabu viwili vya Tanzania bara Azam fc na Yanga ndivyo zilizopata jukumu la kushirik katika michuano ya Klabu bingwa Afrika.
Ushiriki wa vilabu
hivyo umekuja baada ya vilabu hivyo kufanya vizuri katika michezo yao ya mwanzo
ambazo Yanga ilishinda mabao 7-0 ilipokutana na wacomoro kutoka katika visiwa
vya Comoro.
Azam nayo ilishinda kwa
bao 1-0 pale ilipochuana vikali na Klabu moja kutoka Msumbiji.
Matokeo hayo
yameziwezesha timu hazo kuiwakilisha Tanzania katika kushiriki michuano hiyo
inayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ambapo Yanga itamenyana kwa mara ya pili
na Wacomoro hao katika visiwa hivyo.
Azam nao wanatarajiwa
kushuka dimbani siku ya jumapili hiihuko Msumbiji dhidi ya wanamsumbiji kwa
mechi ya marudiano wakitafuta kucheza 16 bora ili waweze kuendelea na michuano
hiyo.
Macho na masikio ya
watanzania ni kwa timu hizo mbili kurudi na ushindi ili waweze kuingia katika
michuano hiyo ya timu 16 bora.
Comments
Post a Comment