Posts

EMMANUEL OKWI AKANA KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUREJEA SIMBA

Image
Baada ya vyombo vingi vya habari kuripoti taarifa Ya Mchezaji wa timu ya Sonderjyske na Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Uganda Emmanuel Okwi Taarifa ambazo KwataUnit.com tumezipata kupitia mtandao wa airtelfootball.ug zinasema kuwa Okwi amekanusha kufanya mazungumzo Ya Kujiunga na Simba. Okwi amesema "Siyo kweli, mimi mwenyewe nimesikia hizo taarifa, akaongeza kwa kusema Hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa na siko katika mazungumzo na Simba. " Okwi mpaka sasa ameshacheza mara 4 pekee katika klabu yake ya sasa ya huko nchini DenMark toka alipoondoka Simba na kujiunga nayo.

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

Image
Mwili unaviungo vingi kama ngozi, Moyo ini, Mapafu na vingine kibao, lakini ndugu msomaji wa KwataUnit.com umewahi kujiuliza kuwa ni Kiungo gani huwa kikubwa zaidi ya Vingine? Kama Ulikuwa hufahamu Tupo kwaajili ya kukufahamisha, NGOZI ndiyo inayotajwa kuwa kiungo kikubwa zaidi, Ngozi ya mtu mzima inakadiriwa kufikia  uzito wa kilo 10.8  na zaidi. Hii Hutegemea na Urefu na Umbo la Mtu pia, lakini mara nyingi hufikia uzito huo, Ngozi hata kwa kuonekana tu huonekana imefunika sehemu nyingi za mwili hasa za ndani, Usikose kuwa unaungana na KwataUnit.com kwa Habari nyingi zaidi.

Hutaamini kiwango cha Bacteria Unachokipata kila unapopigana Denda (Romance),Hii ndiyo idadi..

Image
Kupiga Denda (Romancing)  ni moja kati ya matendo yanayopendwa na watu wengi kwani huamsha hisia za kimapenzi, Lakini umewahi kujiuliza kuwa kuna uwezekano wa kubadilishana bakteria wengi wakati wa tendo hilo? Kwa mujibu wa wataalamu bakteria hao husababishwa na mambo mengi, wengine kiasili hupatikana kwenye mate na wengine husababishwa na mabaki ya chakula yanayobaki kinywani. Sasa wataalamu wanasema unapogiga denda (Romance) unaweza kubadilishana na mwezi wako bakteria kati ya milioni 10 mpaka bilioni 1, upo hapo mwana KwataUnit.com? usikose kuwa unatutembelea kila siku kwa habari mbalimbali.

Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria

Image
Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo. Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea. Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya mashambulizi kuanza. Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.

KINDA AJITABILIA MAZURI

Na Eligius   Nyoni MCHEZAJI kinda wa klabu ya majimaji ya mkoani Ruvuma, Antony Mwingira amesema kwamba licha ya   yeye kuwa ndio mara yake ya kwanza kucheza katika ligi kuu ya Tanzainia ameaidi kufanya mazuri kama atapewa nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.

Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha pauni milioni 50

Image
                 Kwa mujibu wa ripoti, nyota wa Real Madrid, Karim Benzema                         anaweza kujiunga na Arsenal kama wakiweka dau. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akihusishwa na The Gunners ambao hata hivyo bado hawajaonekana kua na dau rasmi la kueleweka. Hata hivyo chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Daily Star kua sasa ni kazi  ya Arsenal  kupigania saini ya nyota huyo kwa dau kubwa ambapo Real Madrid wameripotiwa kumthaminisha kwa kiasi kisichopungua pauni mil 50. Iko wazi kua Arsenal wanaweza kupata ushindani mkubwa wa kumpata nyota huyo kutoka kwa Manchester United ambao nao walionesha nia ya kupata saini. Benzema alikua nje wakati Real Madrid wakitoa sare na Sporting Gijon jumapili hii.

Tetesi: Arsenal sasa macho kwa Cavani.

Image
Kwa mujibu wa sasa Arsenal wanajipanga kwa ajili ya kuipata saini ya nyota wa PSG, Edinson Cavani. The Gunners kwa sasa wanaonekana kua njia panda dili la Benzema, huku kocha Wenger akitia matumaini ya kuipata saini hiyo muda wowote. Huku PSG wakidaiwa kutokua na nia ya kutomuuza Cavani, lakini kitu kinachotia moyo ni kwamba hali ya baadaye kati ya Cavani na klabu haijaeleweka kwa hiyo huenda ukawa ni mwanya mkubwa kwa Arsenal. Cavani ambaye pia alihusishwa na Manchester United mapema mwezi huu, alitua PSG majira yaliyopita akitokea Napoli kwa £55m.