Tetesi: Arsenal sasa macho kwa Cavani.

Kwa mujibu wa sasa Arsenal wanajipanga kwa ajili ya kuipata saini ya nyota wa PSG, Edinson Cavani.
The Gunners kwa sasa wanaonekana kua njia panda dili la Benzema, huku kocha Wenger akitia matumaini ya kuipata saini hiyo muda wowote.
Huku PSG wakidaiwa kutokua na nia ya kutomuuza Cavani, lakini kitu kinachotia moyo ni kwamba hali ya baadaye kati ya Cavani na klabu haijaeleweka kwa hiyo huenda ukawa ni mwanya mkubwa kwa Arsenal.
Cavani ambaye pia alihusishwa na Manchester United mapema mwezi huu, alitua PSG majira yaliyopita akitokea Napoli kwa £55m.

Comments

Popular posts from this blog

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY