Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha pauni milioni 50



                 Kwa mujibu wa ripoti, nyota wa Real Madrid, Karim Benzema
                        anaweza kujiunga na Arsenal kama wakiweka dau.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akihusishwa na The Gunners ambao hata hivyo bado hawajaonekana kua na dau rasmi la kueleweka.

Hata hivyo chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Daily Star kua sasa ni kazi  ya Arsenal  kupigania saini ya nyota huyo kwa dau kubwa ambapo Real Madrid wameripotiwa kumthaminisha kwa kiasi kisichopungua pauni mil 50.

Iko wazi kua Arsenal wanaweza kupata ushindani mkubwa wa kumpata nyota huyo kutoka kwa Manchester United ambao nao walionesha nia ya kupata saini.

Benzema alikua nje wakati Real Madrid wakitoa sare na Sporting Gijon jumapili hii.

Comments

Popular posts from this blog

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY