Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria






Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo.
Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea.

Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya mashambulizi kuanza.

Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.

Comments

Popular posts from this blog

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

MWACHENI MAMA AITWE MAMA

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY