KINDA AJITABILIA MAZURI


Na Eligius  Nyoni

MCHEZAJI kinda wa klabu ya majimaji ya mkoani Ruvuma, Antony Mwingira amesema kwamba licha ya  yeye kuwa ndio mara yake ya kwanza kucheza katika ligi kuu ya Tanzainia ameaidi kufanya mazuri kama atapewa nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.

Mwingira ambaye amekuwa mchango mkubwa katika timu hiyo na kuisababisha  kupanda daraja na kuweza kurudi katika ligi kuu ya Tanzania inayofahamika kama VPL.
Mwingira ambaye kabla ya kujiunga na majimaji alikuwa akizichezea timu za madaraja tofauti ili kuweza kuimarisha kiwango chake kisi potee na klabu ambazo amezichezea  ni Miembeni Fc, Stand Fc, na Magima Fc iliyopo Peramiho mkoani Ruvuma.

Akizungumza na Taifa Letu, Mwingira alisema kwamba yeye ni mchezaji na yuko tayari kwa michezo ya ligi kuu kama atapewa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika timu.
Mchezaji huyo anbaye anapenda kuvaa jezi namba 16, na hakusita kusema mchezaji ambaye anavutiwa nae hapa  nchini ni, Simon Msuva na kule ulaya anampenda Christian Rolnado.

“Mimi ni mwanajeshi, nitakwenda vitani kupambana ili kuakikisha  timu yangu ya majimaji  inashinda kila mechi ambayo nitacheza,.”
Alisema kwamba kila mchezaji ana nafasi ya kucheza katika timu, na ushirikiano kati yake na wachezaji wenzake  wote wanaushirikiano mzuri na wako tayari kupambana.

“Ili kuwa mchezaji bora lazima kufuata yale tunayofundishwa na mwalimu ili tuweze kufanya vizuri katika michezo  yetu  itakayoanza  kutimua vumbi tarehe 12 septemba ambayo majimaji tutafungua daluga letu na Jkt Ruvu katika uwanja wetu wa majimaji hapa mkoani Ruvuma,.”Aliongeza mwingira
  

Comments

Popular posts from this blog

Unajua kiungo kikubwa zaidi kwenye Mwili?, Unajua kina uzito gani? Fahamu hapa

MAMBO YA YANGA NA AL AHLY