Posts

Showing posts from August, 2015

Benzema tayari kutua Arsenal ikiwa tu watatoa kiasi cha pauni milioni 50

Image
                 Kwa mujibu wa ripoti, nyota wa Real Madrid, Karim Benzema                         anaweza kujiunga na Arsenal kama wakiweka dau. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua akihusishwa na The Gunners ambao hata hivyo bado hawajaonekana kua na dau rasmi la kueleweka. Hata hivyo chanzo kimoja kimeliambia gazeti la Daily Star kua sasa ni kazi  ya Arsenal  kupigania saini ya nyota huyo kwa dau kubwa ambapo Real Madrid wameripotiwa kumthaminisha kwa kiasi kisichopungua pauni mil 50. Iko wazi kua Arsenal wanaweza kupata ushindani mkubwa wa kumpata nyota huyo kutoka kwa Manchester United ambao nao walionesha nia ya kupata saini. Benzema alikua nje wakati Real Madrid wakitoa sare na Sporting Gijon jumapili hii.

Tetesi: Arsenal sasa macho kwa Cavani.

Image
Kwa mujibu wa sasa Arsenal wanajipanga kwa ajili ya kuipata saini ya nyota wa PSG, Edinson Cavani. The Gunners kwa sasa wanaonekana kua njia panda dili la Benzema, huku kocha Wenger akitia matumaini ya kuipata saini hiyo muda wowote. Huku PSG wakidaiwa kutokua na nia ya kutomuuza Cavani, lakini kitu kinachotia moyo ni kwamba hali ya baadaye kati ya Cavani na klabu haijaeleweka kwa hiyo huenda ukawa ni mwanya mkubwa kwa Arsenal. Cavani ambaye pia alihusishwa na Manchester United mapema mwezi huu, alitua PSG majira yaliyopita akitokea Napoli kwa £55m.

Haya mengine kuhusu ishu ya Man United na Neymar

Image
Ripoti mpya zinadai kua Neymar atasaini mkataba mwingine wa pesa nyingi klabuni Barcelona na kuachana na uvumi wa Man United Nyota huyo kwa sasa nae amekua akihusishwa sana na Man United huku The Guardian  wakisema kua vyanzo vinadai Neymar anaweza kufikiria kuhamia Red Devils. Hata hivyo mchambuzi mmoja wa La ligaGuillem Balague  ameibuka na kudai kua Neymar anatarajia kuongeza mkataba mwingine na wakali wa Catalan. Mchambuzi huyo ame tweet "Neymar atasaini upya mkataba wake na Barcelona. Lakini kabla hajasaini stori nyingi zitatokea. Ni mchezo wa kizamani"

Uchafuzi wa hali ya hewa wagharimu dola Trilioni 1.6 kila mwaka Ulaya

Image
                                                                                       Uchafuzi wa hali ya hewa. Shirika la afya duniani, WHO kanda ya Ulaya na lile la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, OECD wametoa ripoti yake likisema kuwa uchafuzi wa hali ya hewa barani Ulaya hugharimu dola Trilioni 1.6 kila mwaka kutokana na vifo na magonjwa. Utafiti huo ulitolewa Jumanne wakati zaidi ya wawakilishi 200 wa Ulaya na mashirika ya kimataifa wakikutana Israel kuangalia mustakhbali wa chombo hicho utatumiwa kudhihirisha athari za mabadiliko ya tabianchi kiuchumi. Mathalani ripoti inasema gharama ya kiuchumi kutokana na vifo ni zaidi ya dola Trilioni 1.4....