Wapinzani walalamikia uchaguzi Nigeria
Muhammadu Buhari
Upinzani nchini Nigeria umekosoa
hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi hadi mwishoni mwa Mwezi March.
Chama kikuu cha upinzani cha APC
kimesema hatua hiyo ni kikwazo kikubwa kwa Demokrasia nchini humo.
Chama hicho kimedai kuwa Jeshi la
Nigeria limelazimisha kuahirishwa kwa Uchaguzi ili liweze kumsaidia Rais wa
nchi hiyo, Goodluck Jonathan kwenye Kampeni zake.
Uchaguzi mkuu nchini humo ulipangwa
kufanyika jumamosi ijayo lakini Tume ya Uchaguzi imesema Mashambulizi ya Boko
Haram kwa kiasi kikubwa yanahatarisha uwepo wa zoezi la uchaguzi ,Usalama wa
Wapigakura, na waangalizi wa Uchaguzi.
Hajiya Amina Zakari ni Afisa wa juu
wa tume ya uchaguzi , INEC ameiambia BBC kuwa hawajashurutishwa isipokuwa
walishauriwa kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi.
Kwa upande wake Seneta wa Lawali
Shuaibu kutoka chama cha upinzani cha APC ameiambia BBC kuwa tishio la Boko
Haram sio sababu ya msingi ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment