Alichokijibu Mbunge Mbatia kuhusu ishu ya kusema kuwa Mrema ni mgonjwa.
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP)
alitoa hoja binafsi Bungeni kwamba Mbunge James Mbatia amekuwa akipita
Jimbo la Vunjo na kuwaambia wapigakura wasimchague Mrema kwa sababu ni mgonjwa.
“Napenda
kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo na ninatangaza kuwa
nitagombea tena na hafi mtu hapa“– Alisema Mrema wakati
akimalizia kuwasilisha hoja yake hiyo.
Leo wakati wa kikao cha Bunge jioni, Mbunge
Mbatia alipata nafasi kujibu kuhusu ishu hiyo; “Maelezo haya nayatoa kukanusha kwa moyo wangu wote matamshi
yaliyotolewa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Augustine Lyatonga
Mrema, Mbunge wa Vunjo. Siku ya
tarehe 05/02/2015 wakati wa kuahirisha Bunge Mheshimiwa Mrema alitoa maelezo ambayo sio sahihi alipoeleza
kuwa mimi James Francis Mbatia niliwahi kusema kuwa yeye ni mgonjwa anayeugua maradhi ya ukosefu wa
kinga mwilini yaani UKIMWI“
“Maelezo
yote aliyoyatoa sio sahihi na sijawahi na sitawahi kutamka maneno hayo…
Sijawahi kumnyanyapaa Mheshimiwa Mrema wala mtu yoyote aliyeathirika na maradhi
ya aina yoyote“
“Mimi
sina uadui na mtu yoyote akiwepo mheshimiwa Mrema hata sasa hivi amekaa kwenye kiti changu
sina ugomvi nae. Nimezaliwa na nimekuzwa kwenye familia ya wacha Mungu siwezi
nikafanya hivyo.. To grow old is mandatory but to be wise is optional…”
“Mwaka
huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu ni rai yangu kwa watanzania wote wachague
vionzozi wenye uwezo, wacha Mungu, wakweli na wenye kuchukia propaganda,
ubaguzi, chuki, ubinafsi na ubinafsi“
“Baadhi
ya viongozi wanadai kuwa wana hatimiliki ya maeneo wanayoongoza dhana hii sio
sahihi, nataka kuwahakikishia Watanzania wenye hatimiliki ya nchi yao ni
Watanzania wenyewe.
Comments
Post a Comment