TAHADHARI YA MASHAMBULIZI UGANDA
Polisi wako macho mjini Kampala
Polisi nchini Uganda wamedhibiti
usalama mjini Kampala kufuatia onyo la mashambulizi ya kigaidi kupangwa
kufanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe.
Maafisa wa usalama katika uwanja
huo, walisema kuwa onyo la shambulizi hilo lililopangwa kufanyika Alhamisi
linapaswa kuchukuliwa kwa uzito.
Taarifa
zinazohusiana
1. UGANDA
Marekani ilitoa tahadhari na
kuwashauri raia wake waliokuwa na nia ya kusafiri kwenda nchini humo Alhamisi
kubadili mipango yao.
Kundi la wanamgambo la Al shabaab
lilishambulia mikahawa miwili mjini Kampala mwaka 2010 wakati wa fainali ya
kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Zaidi ya watu 70 waliuawa katika
mashambulizi hayo, wakati ambapo washambuliaji wa kujitoa manga walipojilipua
wakati mashabiki wa soka walikuwa wakitazama michuano hiyo.
"kulingana na taarifa za
ujasusi, kuna tisho maalum dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe na
kundi la kigaidi lisilojulikana. Tisho hilo haliwezi kuchukuliwa kwa wepesi, ''
ilisema taarifa ya maafisa wa usalama.
Taarifa hiyo ilisema kuwa shambulizi
lilipangwa kufanywa kati ya saa kumi na mbili jioni na saa mbili usiku.
Vikosi vya usalama vimeweka vizuizi
katika uwanja huo na katika baadhi ya barabara zilizo umbali wa kilomita 32
kutoka uwanja huo.\
Mikutano kadhaa ya kimataifa
inafanyika nchini humo na lengo la maafisa wa usalama ilikuw akuwahakikishia
usalama wao wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo.
Comments
Post a Comment