Al-Shabaab wamuua mbunge Somalia
Wanamgambo wa al-shabaab wa Somalia
Wanamgambo wa Al Shabab wamedai kuwa
wamemuua kwa kumfyatulia risasi mbunge maarufu mjini Mogadishu.
Ahmed Mohamud Hayd aliuawa baada ya
kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa na katibu wa
Bunge alijeruhiwa,mashuhuda wameeleza.
Taarifa
zinazohusiana
1.Afrika
mashariki
2.Somalia
Kundi la Al-Shabab, ambalo lina
uhusiano na al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi katika kipindi
hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wanamgambo hao walipoteza ngome yao
mjini Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja wa Afrika mwaka 2011,lakini
wameendelea kutekeleza mashambulizi ya mabomu na mauaji mjini humo.
Msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu
Musab amesema kuwa kundi lake limetekeleza mauaji kama ilivyopangwa na kuwa
wataendelea kuwafuatilia Wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge.
Al-Shabab imekua ikipigania kuunda
taifa la kiislamu nchini Somalia.
Comments
Post a Comment