Shughuli ya kupiga kura yaanza Afrika Kusini
Shughuli ya kupiga Nchini Afrika
Kusini ilianza vyema mapema leo asubuhi huku idadi kubwa ya wapigaji kura
ikijitokeza.
Zaidi ya watu million 25 nchini humo
wanaendelea katika vituo vya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu wa mara ya tano
tangu kumalizika kwa utawala wa mtu mweupe.
Taarifa
zinazohusiana na
Chama tawala cha African National Congress,
ANC ndicho kilicho maarufu zaidi. Lakini umaarufu wa chama hicho na rais Jacob
Zuma umeathirika kutokana na tuhuma za rushwa na matatizo ya kijamii.
Licha ya kukumbwa na kashfa za
ufisadi na utawala mbovu, duru zinasema kuwa chama cha ANC huenda kikanyakuwa
ushindi.
Uchaguzi huo unasimamiwa na maafisa
zaidi ya 200,000 wa tume ya uchaguzi watakao zunguka mikoa yote 9 iliyoko
nchini.
Comments
Post a Comment