KLABU YA LIVERPOOL WAPOTEZA MATUMAINI YA KUPATA UBINGWA
Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier
likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace .
Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa mbele
kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma bila bao huku
wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool.
Taarifa zinazohusiana
Michezo
Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka
mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu.
Lakini Damien Delaney na Dwight Gayle walipunguza
pengo hilo na kuingiza mabao matatu katika muda wa dakika mbili katika kipindi
cha pili cha mechi.
Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa
wazi wasijuie cha kusema.
Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja
tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza.
City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa
Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi
ya West Ham Jumapili.
Comments
Post a Comment