Kikosi cha Marekani kusaidia Nigeria
Marekani imetangaza kwamba imetuma
kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana takriban 200
wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji
nyara wa wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja
ili kulikomesha Boko Haram.
Taarifa
zinazohusiana
"Tayari tumetuma kundi letu
Nigeria. Wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wanajeshi, wadumishaji wa
sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili
wawape msaada," Rais Obama alisema.
Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa
inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana
na kuangamiza Boko Haram.
Nchini Rais wa Nigeria, Goodluck
Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake, Daktari Reuben
Abati.
"msaada huo kutoka kwa Rais Obama
uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa tisa alasiri
hivi," Daktari Abati alisema.
Comments
Post a Comment