Posts

Showing posts from May, 2014

Shughuli ya kupiga kura yaanza Afrika Kusini

Image
Shughuli ya kupiga Nchini Afrika Kusini ilianza vyema mapema leo asubuhi huku idadi kubwa ya wapigaji kura ikijitokeza. Zaidi ya watu million 25 nchini humo wanaendelea katika vituo vya upigaji kura kwa uchaguzi mkuu wa mara ya tano tangu kumalizika kwa utawala wa mtu mweupe. Taarifa zinazohusiana na Siasa Chama tawala cha African National Congress, ANC ndicho kilicho maarufu zaidi. Lakini umaarufu wa chama hicho na rais Jacob Zuma umeathirika kutokana na tuhuma za rushwa na matatizo ya kijamii. Licha ya kukumbwa na kashfa za ufisadi na utawala mbovu, duru zinasema kuwa chama cha ANC huenda kikanyakuwa ushindi. Uchaguzi huo unasimamiwa na maafisa zaidi ya 200,000 wa tume ya uchaguzi watakao zunguka mikoa yote 9 iliyoko nchini.

Kikosi cha Marekani kusaidia Nigeria

Image
Marekani imetangaza kwamba imetuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia kuwatafuta wasichana takriban 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na wapiganaji wa kundi la Boko Haram. Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kulikomesha Boko Haram. Taarifa zinazohusiana "Tayari tumetuma kundi letu Nigeria. Wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wanajeshi, wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada," Rais Obama alisema. Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kutumia utekeji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana na kuangamiza Boko Haram. Nchini Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amekubali msaada huo kama alivyosema msemaji wake, Daktari Reuben Abati. "msaada huo kutoka kwa Rais Obama uliwasilishwa na Waziri wa Mashauri ya Kigeni John Kerry kama saa t...

KLABU YA LIVERPOOL WAPOTEZA MATUMAINI YA KUPATA UBINGWA

Image
Liverpool wameona giza huku kombe la Ligi ya Premier likiwakwepa baada ya kwenda sare ya mabao matatu dhidi ya Crysral Palace . Cha kushangaza ni kwamba Liverpool walikuwa mbele kwa mabao matatu lakini Cyrstal walitifua kivumbi na kutoka nyuma bila bao huku wakimaliza mechi kwa mabao matatu sawa na Liverpool. Taarifa zinazohusiana     Michezo Joe Allen, Daniel Sturridge na Luis Suarez waliiweka mbele klabu yao katika muda wa saa moja kwa mabao matatu. Lakini Damien Delaney na Dwight Gayle walipunguza pengo hilo na kuingiza mabao matatu katika muda wa dakika mbili katika kipindi cha pili cha mechi. Hali hii iliwachaa mashabiki wa Liverpool vinywa wazi wasijuie cha kusema. Liverpool sasa wako mbele ya Man City kwa poiti moja tu kwenye jedwali la alama.City bado wako na mechi moja kucheza. City watamenyana na Aston Villa katika uwanja wa Etihad mnamo siku ya Jumatano, kabla ya kumaliza msimu kwa mechi nyingine dhidi ya West Ham Jumapili. ...