Hatimaye muda umefika. Al Ahly tayari wapo jijini. Kwa mashabiki wa Yanga, ni wakati wa hisia mchanganyiko. Furaha iliyojichovya kwenye woga wa kukutana na timu kubwa. Kwa upande mmoja wasingependa kukutana na wababe wao katika raundi ya kwanza. Kwa upande wa pili, timu kubwa kama Alhly hupandisha mzuka kwa mashabiki. Ni fursa nyingine tena kwa Yanga, aidha kufungua ukurasa mpya kwa kuwafunga wamisri kwa mara ya kwanza au kuendeleza uteja kwa waarabu. Mechi sita, vipigo vinne, kapu la magoli 14 huku wakijitutumua kwa kufunga bao moja ni historia ambayo kila Mwanajangwani asingependa iendelee hio Jumamosi. Mara ya mwisho, timu hizi zilipokutana, Al Ahly walimaliza biashara kwenye mechi ya kwanza tu kwa ushindi wa 3-0 huko Cairo. Kipigo cha ‘tatu bila’ kilipelekea kocha wa Yanga wa wakati huo, Dusan Kondic kuinua mikono na kukiri ‘kiroho safi’ tu kuwa Al Ahly wapo anga zingine na Yanga hawawezi kushinda hata mechi ya marudiano nyumbani. Mechi ya marudiano hapa Dar,...
Comments
Post a Comment