Mtoto mkubwa azaliwa Marekani
Avery mtoto mkubwa kuliko kawaida
nchini Marekani
Mwanamke mmoja nchini Marekani
amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1 sawa na kilo 6.4kg na sasa mtoto
huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto mchanga .
BiMaxxzandra Ford amepata mtoto
aliyempa jina Avery, ndiye mtoto mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika
hospitali ya wanawake ya mtakatifu Joseph iliyoko Tampa, Florida.Avery,
alizaliwa kwa njia ya kawaida .
Ford alikuwa hajatanabahi kuwa yu
mjamzito mpaka alipotimiza wiki 35 .lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito
kupita kiasi ,madaktari wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi
ya unenepaji mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe sivyo.
Debbie Moore, mkunga katika
hospitali hiyo, wasingemruhusu mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida kama
wangegundua mapema ana mtoto mwenye kilo nyingi kiasi hicho .
Avery anabaki hospitalini chini ya
uangalizi maalumu tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini anatarajiwa
kuruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni .
Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye
umri wa mwaka mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.
Comments
Post a Comment