'SIMBA SC. HONGERENI NA KILA MTU AWAJIBIKE KWA NAFASI YAKE'

Dar es Salaam SIMBA SC ni klabu kongwe ambayo watu wengi wanategemea ipate mafanikio waka wowote, lakini msimu wa mwaka jana na msimu huu imesuasua sana na kuwanyong`onyesha mashabiki wake waliokuwa na matarajio makubwa na kikosi chao. Katika maisha ya kawaida, kuna wakati mambo yanakuwa safi na kuna wakati mambo yanakuwa magumu. Kipindi cha mpito huwa kinatokea, na ndio maana kuna muda unaweza kuwa na pesa nyingi na kufurahia maisha, lakini ikafika wakati ukakosa hata mie moja. Kimsingi inapotokea hali mbaya kwako ndio kipimo chako, na jamii itahitaji kuona jinsi unavyokabiliana na changamoto yako. Mtandao huu ulifanya mahojiana na katibu mkuu wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga ambaye kwa asilimia kubwa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za klabu. Katika mahojiano hayo, Kamwaga aliwatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa klabu haina mgogoro wowote baina ya benchi la ufundi na wachezaji, au viongozi na benchi la ufundi au viongozi na wachezaji. Kamwaga alibainisha kuwa hal...